KAMPUNI ya mawasiliano ya Zantel imezindua ofa maalumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake.

Ofa hiyo itawawezesha kufanya mawasiliano kwa gharama nafuu sambamba na kupata taarifa muhimu kuhusu kipindi cha mfungo.

Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano na Habari wa Zantel, Rukia Mtingwa, alitangaza ofa hiyo mjini Zanzibar.

Amesema, “Ramadhan ni muda muafaka wa kujenga uhusiano mzuri na ndugu, jamaa na marafiki, ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao na kupata taarifa muhimu za mwezi huu mtukufu”.

Mtingwa alisema ofa hiyo ya Ramadhan, imelenga kuwazawadia wateja wa Zantel, watakaojiunga na vifurushi mbalimbali vya muda wa maongezi vya siku, wiki na kifurushi cha mwezi.

Wateja ambao wataweka kifurushi cha muda wa maongezi wa Sh 999 kila siku wataweza kupata ujumbe wa maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, ujumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, ujumbe wa kukumbusha wakati wa swala 5 na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran Takatifu.

Alisema wateja watakaoweka kifurushi cha wiki cha Sh 4,999, wataweza pia kupata ujumbe wa maneno ya bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, ujumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, ujumbe wa kukumbusha wakati wa swala 5, kuwakumbusha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran Takatifu.

Hali kadhalika wateja wataoweka kifurushi cha mwezi cha Sh 14,999 wataweza kupata ujumbe wa maneno za bure kati ya mtandao wa Zantel kwa Zantel, ujumbe mbalimbali kuhusu mwezi wa Ramadhan, ujumbe wa kukumbusha wakati wa swala 5, kuwafahamisha muda wa kufuturu na nukuu mbalimbali za maandiko ya Kuran Takatifu.